Mamba fc ya kaloleni iliweza kutawazwa mabingwa wa kombe la otty father awamu ya kwanza baada ya kuwanyuka maasidi wao wa jadi hakat fc kutoka makadara bao moja kwa bila katika uwanja wa camp toyoyo jijini nairobi.
Katika mechi za nusu fainali, mamba walisajili sare ya mabao 2-2 walipochuana na Amasa fc na kuweza kuwabandua kupitia matuta ya penalti nao hakat fc wakaweza kuwaadhibu sinema bao moja kwa bila na kuweza kujikata tiketi ya kucheza fainali.
Fainali hiyo ambayo ilihudhuriwa na lukuki ya mashabiki wa soka kutoka jiji la nairobi ilikuwa ya kusisimua huku kipindi cha kwanza timu zote zikisajili sare ya kutofungana.


RELATED ARTICLES


Katika kipindi cha pili mshambulizi wa timu ya black mamba fc erick mata ambaye pia alituzwa tuzo la mchezaji bora wa mashindano hayo na vilevile mfungaji bora aliiweka mamba fc kifua mbele, bao ambalo liliwapa ushindina kubeba kombe la otty father.
Akizungumza na dawati la sporta, nahodha wa timu ya black mamba gregory onyango alisema kwamba licha ya mechi kuwa ngumu ushirikiano mwema wa wachezaji wenzake uwanjani pamoja na nidhamu ndio uliochangia ushindi huo.
“Mechi ilikuwa ngumu hasa katika kipindi cha kwanza,hatukushuhudia mabao lakini kipindi cha pili nliwaambia vijana wangu jambo la kufanya na waliporudi uwanjani walitekeleza nliyowaambia na kuweza kupata bao moja ambalo lilikuwa la ushindi.Namshukuru Mungu kwa kuweza kushinda mashindano haya awamu ya kwamza , sahii tunajiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya kaunti ya nairobi na natumai vijana wangu watafanya vizuri”, kauli yake kocha wa mamba fc.

Timu hizi mbili ziliwahi kushiriki katika ligi ya juu humu nchini kpl miaka ya alfu moja mia tisa sabini na themanini.