Kwa mara ya kwanza kenya kushiriki katika michuano ya kombe la bara Afrika ilikuwa ni mwaka wa 2004 wakati ambapo wachezaji kama vile robert mambo, musa otieno , simon seppe mulama, denis oliech na wengineo,walikuwa wakihudumia timu ya taifa harambe stars.


RELATED ARTICLES


Mipango kabambe wakati huo ilikuwa imewekwa na timu hiyo iliyokuwa na muingiliano mzuri kutokana na kipindi kirefu ambapo wachezaji hao walikuwa wakicheza pamoja.
Robert Boban Mumba Mambo, ambaye alichukua beji ya unahodha wa timu ya taifa harambee stars kutoka kwa Musa Otieno, katika mahojiano ya kipeke na dawati la michezo la sporta anatueleza kwamba ili kuweza kuimarisha soka nchini jambo la msingi ni kuanza kukuza vipaji vya wachezaji wakiwa wangali wadogo na hili litapatikana ikiwa mipango kabambe itaweza kuwekwa na wahusika wa michezo nchini.

Hilo likiweza kufanyika huenda kenya ikashiriki tena katika mashindano ya kombe la bara africa na vilevile ata kuweza kujikatia tiketi ya kushiriki mashindano makubwa duniani, kombe la dunia.