Watani wa jadi afc leopard na gor mahia wanatarajiwa kuumiza nyasi hapo kesho katika uwanja wa nyayo jijini nairobi katika mechi za ligi kuu nchini kpl.

kogallo ambao ni mabingwa mara 15 wanaonoza jedwali la msimmo wa ligi wakiwa na pointi 43 huku maasidi wao leopards ambao ni mabingwa mara 13 wakishikilia nafasi ya 12 kwa pointi 23.

Katika msururu wa kwanza vijana wa gor waliwalaza afc mabao 3 bila jibu katika uwanja huo wa nyayo swali likiwa ni je, wanachui watakubli tena kichapo kutoka kwa gor?

Na katika mechi tano za mwisho ambazo mashemeji wameweza kushiriki gor mahia wameweza kushinda mechi 3 kutoka sare mechi mbili na kupoteza mechi moja dhidi ya leopard wakiwa wanapigiwa upato kutokana na matokeo bora wanaoonyesha.