Ligi kuu ya kenya “sportpesa premier league” msururu wa 13 unatarajiwa kushuhudiwa leo katika viwanja mbalimbali kabla ya kuenda mapumziko ya wiki mbili ili kuweza kupisha mechi za kimataifa ambazo zitakuwa zikishuhudiwa juma lijalo kwa mujibu wa kalenda ya Fifa.
Kenya ilifaa kuchuana na Angola katika uwanja wa machakos lakini mechi hiyo imetupiliwa mbali.
Wadhamini wa ligi kuu,wameweza kuandaa mashindano ya sportpesa cup ambayo yatakuwa yakishuhudiwa katika uwanja wa taifa wa Benjamin Mkapa nchini Tanzania miongoni mwa timu ambazo zinadhaminiwa na kampuni hiyo.
Kenya watawakilishwa na timu ya gor mahia, afc leopard, mabingwa watetezi wanmvinyo tusker pamoja na vijana wa nakuru all stars.
Timu ambayo itakuana na klabu ya everton ya England itachaguliwa katika mashindano hayo.
Jumamosi hii , nzoia sugar wataziumiza nyasi dhidi ya sofapaka katika uwanja wa mumias compex, thika united wavaane na vijana wa muhoroni katika uwanja wa manispa ya thika, wawakilishi wa ukanda wa pwani bandari fc watawakaribisha kakamega homeboyz katika uwanja wao wa nyumbani wa mmbaraki nao chemelil sugar wamalize udhia wa mechi za leo kwa kuchuana na ulinzi stars katka usanchari wao wa chemelil.
Siku ya jumapili zoo kericho ambao wamepanda ngazi kwenye ligi kutoka supa watavaana na wanasukari sony sugar katika uwanja wa green stadium, western stima wakipige dhidi kariobangi sharks katika uwanja wa moi jijini kisumu,mathare united watakuwa ugenini dhidi ya nakumatt katika uwanja wa nyayo, tusker wawe wenyeji wa mabingwa mara 13 Afc leopard katika uwanja wa kinoru,nao viongozi wa jedwali gor mahia watamaliza udhia wa mechi za jumapili dhid ya vijana wa pamzo posta rangers
Mechi zote zimeratibiwa kugaragazwa mwendo wa saa tisa mchana saa za Afrika mashariki.

JEDWALI LA LIGI KUU YA SPORTPESA

Nambari timu P W D L GF GA GD Pts
1 Gor Mahia 12 8 2 2 17 7 10 26
2 Ulinzi Stars 12 7 3 2 18 10 8 24
3 Tusker 12 7 3 2 16 12 4 24
4 Posta Rangers 12 6 5 1 9 4 5 23
5 Kariobangi Sharks 12 6 2 4 11 8 3 20
6 Sofapaka FC 12 5 4 3 13 8 5 19
7 Bandari FC 12 5 2 5 15 11 4 17
8 Kakamega Homeboyz 12 4 5 3 7 6 1 17
9 Nzoia United 12 4 4 4 17 13 4 16
10 Nakumatt 12 4 4 4 10 10 0 16
11 AFC Leopards 12 4 3 5 10 12 -2 15
12 Chemelil Sugar 12 3 5 4 9 9 0 14
13 Sony Sugar 12 4 2 6 8 12 -4 14
14 Zoo Kericho 12 3 3 6 10 16 -6 12
15 Muhoroni Youth 12 2 4 6 7 14 -7 10
16 Thika United 12 2 3 7 11 17 -6 9
17 Mathare United 12 2 3 7 9 18 -9 9
18 Western Stima 12 2 3 7 8 18 -10 9

Na sam obura