Mabingwa watetezi wa ligi kuu humu nchini kpl tusker fc wanatarajiwa kuingia uwanjani jumapili hii kukabiliana na mathare united ambao wanashikilia nafasi ya 15 kwa alama 9 baada ya kucheza mechi 11.
kpl
Licha ya vijana wa kocha George nsimbe, raia wa Uganda kuanza msimu vibaya, kwa sasa kikosi chake kinashikia nafasi ya nne wakiwa na alama 21 na jumapili watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya mathare united ambao watakuwa wakicheza nyumbani.
‘ni lazima tushinde mechi za ugenini ndiposa tuweze kuhifadhi taji ambalo tulililshinda msimu jana, haitakuwa rahisi, na wikendi hii itatulazimu tushinde mechi yetu ya ugenini dhidi ya mathare’, alisema kocha huyo.

Kwengineko vijana wa Stewart hall afc leopard watakumbwa na kibarua kigumu siku ya jumamosi watakapokabiliana na kakamega homeboyz ambao msimu jana waliwaadhibu mabao manne kwa moja.

mechi zIngine ambazo zatarajiwa kugaragazwa wikendi hii:
JUMAMOSI:
muhoroni youth watavaana na nzoia sugar
nakumatt fc waichape dhidi ya wanasukari chemelil sugar
sofapaka wavaane na kariobangi sharks
nao wawakilishi wa ukanda wa pwani bandari fc wakipige dhidi ya zoo kericho ambao wamepandishwa ngazi kushiriki ligi kuu msimu huu kutoka ligi ya supa.

JUMAPILI
Sony suga watacheza dhidi ya western stima
ulinzi stars wavaane na posta rangers
nao mabingwa mara 15 gor mahia wamalize udhia dhidi ya thika united katika uwanja wa nyayo.