Jina Ali mohamed sio geni kwa vichwa vya wengi, kwani kuna watu wengi mahiri wenye jina sawa na hili ambao wameweza kutamba katika nyanja mbali mbali za michezo kama vile aliyekuwa mwana masubwi wa marekani na wengineo.

Katika safari yangu kwenye kaunti ya mombasa hususan katika eneobunge la mvita, nakutana na kikosi cha watoto wenye chini ya umri wa miaka 15 wakiwa mazoezini muda wa jioni uwanjani sunni serani.
vlcsnap-2017-05-19-09h08m33s207

Vijana hawa wa timu ya future stars wapo chini ya nahodha wao mahiri Mohamed Ali, ambaye kila siku baada ya wanafunzi kutoka shuleni huwa anahakikisha wachezaji wenzake wanafika uwanjani kwa wakati ufaao ili kuchapa mazoezi ya kishua kabla ya kuswali swalaah ya maghrib.

‘lengo langu kuu kama nahodha ni kuhakikisha kwamba wachezaji wanakuwa na nidhamu uwanjani,wanafuata sheria za soka na kuweza kushirikiana kwa umoja wakati wakicheza na timu pinzani’.

Shabiki huyu sugu wa timu ya mashetani wekundu manchester united,kwa jinsi anavyoipenda soka ya wayne rooney ana ndoto za kuchezea timu hiyo siku za usoni.

Mwenyekiti wa jamii ya wa sunni ambaye pia aliwahi kuichezea timu ya congo boyz miaka ya tisini,kila siku huwa yupo uwanjani kuwapa makinda hao sapoti na mafunzo ya soka.

‘Malengo na madhumuni ya kuwaleta vijana hawa pamoja ni kuwa sahii ukiangalia mombasa yetu ilivyokuwa watoto wengi wamepotea kwenye madawa za ulevya, uhalifu na mambo mengine ambayo hayana msingi mwema kwenye jamii,ndio tukaja na fikra hii sisi kama wachezaji wa zamani kutengeneza kikosi cha vijanawenye chini ya umri wa miaka 7 na 12.

Mkoa wa pwani unajulikana kwa kuweza kukuza wachezaji bora ambao wameweza kuichezea timu ya taifa akiwemo KENYA 1 Abas mohamed,aliyekuwa kocha wa bandari twihir muhiddin na wengineo na sasa macho yapo kwenye kinda huyu wa future stars,Ali ambaye ndoto zake za kuchezea manchester united zikitimia basi ataingia katika vitabu vya kumbukumbu kuchezea timu ya England baada ya Victor Mugubi Wanyama anayeisakatia timu ya tottenham hotspurs.